[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

WALE 144000 WALIOKO MLIMANI SAYUNI

 

Ufunuo wa Yohana 14.

1 Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya Mlima Sayuni, na watu mia na arobaini nanne elfu pamoja naye,  wenye jia lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao; 3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wane, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwakatika nchi. 4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5 Na katika vinywa vyao haukunekana uongo. Maana hawana mawaa.

PDF

Macho ya ndani ya Mtume Yohana yalifunguliwa yakaweze kuona maono ya ajabu yanayofunuliwa machoni pa mataifa hata wakati huu tuliomo. Aliupata ufunuo mkuu la kundi tukufu la mia na arobaini na nne elfu waliokuwemo Mlimani Sayuni. Lakini hili sio kundi tu lenye hesabu Fulani. Huu ufunuo wa kundi hili ni uashirio wa wale waliokombolewa na Mungu, na hili ono hufanyika na kuendelea kufanyika hata milele, ikiwa ni jambo linalofanyika wakati huu na kuendelea hata vizazi na vizazi. Hili kusanyiko la kimbingu hufanyika wakati mwanadamu anapojivumbua kutokana na kushikamana kwa utope wa kuishi kiwanadamu, na kuanza kukwea na kupaa kurejelea utukufu wake uliohitimishwa kwenye upeo wa Ufalme wa Mungu.

Kilele cha Mlima Sayuni – ambacho ni furaha na tumaini la vizazi visivyohesabika, ni ni upeo wa kiroho ulioinuka na kukwezeka, mahali ambapo Ufalme wa Mungu – mji wa Milele wa Mungu Aishie, ambo kwa jina jingine waitwa Jerusalemu ya Kimbingu wapatikana. Klele hiki chaashiria chanzo na hatima ya kila kiumbe, ambapo kila kilicho hai huwa na chanzo chake na pia huhifadhika; mahali paishipo Uwepo usiopimika, Nguvu na Utukufu wa Mungu Aishie.

Hili kusanyiko ling’aalo Mlimani Sayuni, ni kweli fulani iliyoko hata wakati huu tuishio, wala sio jambo lijalo wakati fulani wa siku za usoni, vile wengi wetu wamefanyika kusadiki. Ni hali ilioko ambayo ina utukufu, na ambayo Mungu anatamani kila mwanadamu akaweze hitimia, Ufalme wa Amani kamilifu, utangamano na Utukufu. Ulimwengu unapoyumba mbele na nyuma kwa kukosa uhakika na kujawa na uoga, unapoyumba kwa ulevi wa uongo wake, kubobea, kunawiri na amani ya mahali hapa patakatifu pazidi kutotikiswa wala kutetemeshwa milele.

Kila mwanadamu mwenye roho wa kupambanua mambo na ambaye kwa ujasiri ataisikia sauti ya Yeye Ambaye Ndiye Mchungaji Pekee wakati huu, atajipata akitembea katika hali hii iliobarikiwa, kileleni mwa Mlima Sayuni, kati ya wale Mia na Arobaini na Nne Elfu, waliokombolewa toka kati ya wanadamu. Sauti iliyo nyororo inayosikika katika vilindini vya mtu aliyekwepa uzembe rohoni, itamwongoza na kumshauri kutoka msimu wa kiza hadi msimu wa nuru, mahali ambapo kifo, kilio na huzuni havimo tena.

Hawa waliokombolewa wasimama kama nuru ya ulimwengu – wao ndio Yerusalemu Mpya inayoshuka, kufunua uzuri wake wa kimbingu mbele ya macho ya ulimwengu wote, kwa utukufu na heshima ya Aliyewaita na kuwatwaa kutoka kizani kuingia katika Nuru Yake Kuu.

Katika maono haya makuu ya kimbingu, Roho afunua hali tukufu ya wae ambao watahitimu kuingia katikahali hii ya ya ukamilifu na ututkufu usio kipimo ndani ya na kama Mwana ambaye ndiye Kristo.

Mia na Arobaini na Nne elfu yamaanisha nini?  Mia na Arobaini na Nne Elfu (ambayo ni 12 X 12 X 1,000) ni nambari inayoashiria Wana. Israeli kama taifa liliundika kwa jamii kumi na mbili. Wanafunzi wa Yesu pia walikuwa kumi na wawili. Inaashiria wana wa Ufalme ambao wamefikia ukamilifu wa hatima ya kimbingu ya Kristo. Kiroho, 1000 ni nambari inayotumika kuashiria kitu kisicho kipimo. Lazima tuwe maakini ya kwamba mambo yanayohusu Mungu na Ufalme Wake, hayawezi nakilika wala hesabik kutumia vipimo vya kiwanadamu kama wakati na muda, idadi wala kiwango; Mungu hutumia hivi vipimo kama viashirio na ishara za kudhihirisha hisia Zake zikilinganishwa na hali Yake ya kutoonekana, kufichika kwake, na Umilele wa Ufalme Wake. 

Wale wajipatao Mlimani Sayuni, kati ya umati wa waliokombolewa kutokana na kukamatwa na nguvu za kifo, mauti na uharibifu na wanasimama katika uhuru mtukufu wa wana wa Mungu, wakiwa huru kutokana na nguvu za dhambi na dhamiri iliyosongeka. Hawa husimama bila najisi mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu katika upendo bila chembe yeyote ya kuhukumika wala dhamiri ya dhambi; wanaishi katika uwepo wa Utukufu Wake. Hiki ndicho kilele cha kiroho cha uwepo mkuu Mungu, mahali ambapo Bwana amekuja kuwakusanya watafutao wokovu wake. Kwa ajili ya hili, Baba kupitia sauti ya Mwana asema: Nitarejea kuwakusanya, ili NILIPO, nyinyi muwe pia; huu ndio mwito ulioinuliwa uwaitao wanadamu wawezao kusikia wakiitwa kushiriki wakati na saa kama sasa.

Kuelewa kwetu kunapoimarika, na mwanadamu anafanyika zaidi na zaidi kupsmbsnukiwa na najisi iletayo uharibifu, twahimizwa kuitorokea ile najisi iletayo uharibifu na kuukwe mlima ulioinuka.

Marko 13

 

14 Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;

Mungu anapeana ishara hii ya kiroho kwa wapenzi wake walio na masiki ya kusikia kile Roho asemacho. Chukizo la uharibifu ni umbo la mnyama Yule na jka lile ambalo ni mtu wa dhambi lisimamalo kwenye mahali pa Mungu ndani yetu (kwani sisi tu Hekalu ya Mungu) wakati wanadamu walilala katika kiwiliwili sha kuwa wao ni watu wa jinsia. Yesu asema kwa wana wanaoweza kuipambanua kweli, kwamba nuru ya ufunuo wa Kristo inapong’aa, mzifungue nafsi zenu kutokana na kila hali ya kusongwa na Shetani ambayo imewafunga kwa jela la utu batili wa kijinsia na ukaweze kupaa Mlima wa kiroho wa Mungu, uitwao Sayuni. Wale ambao, kwa uvumilivu watamfuata Mwana-Kondoo katika kizazi hiki kutokana na hali inayokufa ya mwanadamu wa kijinsia, ambayo wameishikilia kwa muda wa maisha yao yote, kuingia kwa umbo la kiungu la mwana wa Mungu, ni wale ambao watajipata Mlimani Sayuni, wakiwa wamenunuliwa kutokana na wanadamu walio duniani. Kila mwanadamu ameitwa akaweze kuhama kutoka sehemu za chini za kilimwengu, mahali ambapo hali ya kutofahamu hutamalaki, na akaweze kukwea na kuingia Mimani mwa Mungu. Makusudi ya Mungu ni kuwanunua wanadamu wote na kuwakusanya tena Mlimani wake Mtakatifu Sayuni, mahali ambapo walianguka kutoka.

Kununua huku kuna maana gani? Kunamaanisha kuwaleta watu wake kutoka uharibifu hadi mahali pa Baraka, yanena kuhusu wokovu, kulindwa, kuwekwa muhuri, kufunikwa naye, urejesho, kupendwa, kuonyeshwa rehema nk. “Ndio”, hawa wamenunuliwa kutokana na wanadamu na wakakwezwa kutokana na hali iliyodhoofika ya mwanadamu wa kijinsia kuingia katika hali ya umilele ya wana wa Mungu. Watu hawa wa uzao spesheli sio watu wa jinsia ya wanadamu wa ulimwengu wa kawaida. Uzao wao hauwezi kunakiliwa kutoka kwa ratiba ya uzao wa wanadamu, wao wanaishi kutokana na uzao wa Melkizedeki ambaye hana baba wala mama.Wameshinda minyororo na pingu za uharibifu na kupaa kwa uhuru na usafi war oho zao.  Wanapojitambua tena ndani ya utukufu wa Baba yao kwa kununuliwa kwao kwa damu ya Mwana-Kondoo, hawa waliofanyika haki wa Mungu wanaenenda wakifanyika dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani kote ili wote wakawatizame. Wanafanyika ishara na vibango vya kuashiria ili kila mwanadamu waone, waamini na kubadilika kuwa kama mfano wa Mwana; wanafanyika kuwa wakombozi wa wana wengine walio kwenye vifungo vya uharibifu na kifo. Hali yao ya kukwezwa na kutukuka katika Kristo inawafanya wao kufanyika makuhani wa milele wa Mungu aishie, na wanafanyika mpito na daraja kati ya wanadamu na Mungu Baba yao; na wanatamalaki na kutawala kama wafalme wakieneza uzima na haki kwa wanadamu wote.

Warumi 8

19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vyoe pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika tumaini; 21 kwa kuwa vuimbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa kaika utumwa wa uharibifu, hta viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

Kama ushawahi kujionea sinema maarufu ya Uamerikani iitwayo  "Superman", ushawahi basi chungulia katika mipango ya umilele ya Mungu; wale wanadamu waliozitengeneza sinema kama zile hupatiwa maono fulani ya kiungu hata bila yao kujua na kuyaleta yale maono mazito na kweli za kiroho kwa njia iliyofichika kwa wanadamu. Sinema yenyewe huanzaje? “Ni tai, ni ndege, la, ni Superman”. Mungu anauinua Mwili wenye viungo vingi unaoonyesha na kufanya kazi zile haswa zinazofanywa na yule ‘Superman’ kwa ile sinema. Kazi za kutetea kweli, haki na uhuru wa wanadamu wote, kutenda kazi nzuri za ukombozi na kudhihirisha nguvu za Mungu kwa utukufu wake Baba.

Johana 1

12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Wengi wamesoma sura hii na mstari huu kwa biblia, lakini hawajauelewa kwa hakika. Nguvu ya kufanyika mwana wa Mungu ni mamlaka na uhuru wa kutenda kwa uhakika kama Mungu hapa duniani. Ni maana kuwa, kuwatizama hawa wasimamao Mlimani Sayuni, ni kama kumtizama Yeye Pekee Mungu; hamna mwanadamu ambaye ashawahimwona Mungu Baba kimwili, lakini hawa wana wa Mungu wanamdhihirisha – wanamfunua akaonekane.

 


 

JINA LA BABA KWA VIPAJI VYA NYUSO ZAO

Katika maono yake, Yohana pia aligundua kwamba Jina la Baba lilikuwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso za watakatifu ambao walikuwa wamenunuliwa kutokana na uso wa ulimwengu. Ndugu zangu, kuna majina mawili tu yaliyotajwa kuwa yameandikwa vipajini mwa nyuso za watu; nayo ni – Mhuri - Jina la Baba, na mhuri wa Yule mnyama – jina la yule nyoka wa zamani ambaye ni yule mnyama. Hatupaswi kutishwa na ukubwa wa maneno kama ‘yule myama’, ‘nyoka yule’ ama ‘joka lile’ ambayo yametumika mara kadhaa ndani ya kitabu cha Ufunuo, kwa sababu, yote hayo yaashiria mambo mengine tofauti. Kwa majina haya, ni mwanadamu ambaye anaashiriwa akisimama kama uzao wa Mungu ama uzao wa Shetani. 

Mhuri wa Yule mnyama ni ujumbe ambao unaweza tu tajwa katika kijitabu hiki. Wakati ule tu mwanadamu alilila lile tunda la maarifa na ujuzi wa mema na mabaya, ambalo lililetwa kwake na yule nyoka (mwerevu kuliko wamyama wote wa mwitu), aliandikika ile nambari ya yule mnyama. Ile nambari ya yule mnyama ni sambamba na ile hali ya yule nyoka; twayaona haya katika Mwanzo kwa sababu yule nyoka ndiye aliyekuwa mwerevu kuliko wamyama wote wa mwitu ambaye aliwaandika wanadamu kuanzia Mwanzo katika kuasi kwa mwanadamu. Kuanzia pale hata hadi siku hii tulioko, kiburi, na hisia ya kujiona imekuwa hli ya ukawaida wa mwanadamu, aliiridhi dhamiri ya dhambi inayoasi, inayoashiriwa katika Mwanzo na uchi wa Adamu mbele ya uwepo wa Mungu. Na ndio maana Yesu, bila kuchanganya maneno akawaita wale waliompinga uzao wa nyoka, kumaanisha kuwa walikuwa na mhuri wa yule mnyama juu yao.

Kuanzia wakati ule wa uasi wa mwanadamu, yeye amekuwa akikwepa na kuuondokea uwepo wa Mungu na akaupoteza uweza, mamlaka na uridhi kama mwana wa Mungu katika nuru. Tulichoshuhudia katika shamba la Edeni ni mwanadamu, akishuka kutoka kilele cha uwepo wa Mungu Mlimani Sayuni kuingia katika uvumbi wa dunia mahali ambapo yule nyoka alitawala. Katika uhai, mwanadamu huvalia umbo na mfano wa mtu wa mavumbi. Jua kwa hakika kuwa lile fumbo la majaribio ya Adamu na kuasi kwake, anapojiambatanisha na cha kimwili na cha jinsia, yeye hukana kwa yale matendo uungu wake, ambao na huru, usioharibika na wa milele, kuanzia Mwanzo.

Lakini twashukuru Mungu kwa sababu, kupitia damu ya Mwana Kondoo, tuna njia ya kurejea kwa utukufu ambao wote wameupotea kupitia Adamu, huo utukufu usiodhoofika wa Baba uliopotewa kutoka misingi ya dunia. Kila mtu leo amepewa neema ya kutosha ya kumsababisha kupaa kutoka vilindini mwa dunia, hata kwa Mlima Sayuni mahali ambapo utukufu wa Mungu na uwepo wake uko na waishi. Huo muhuri  wa Yule mnyama ulioko kwenye  kipaji cha uso ambao wakati wote umemhusisha mwanadamu na Shetani na ufalme wake usio haki hufutwa na jina na hali ya uzima wa Baba unafuniliwa, ukiwa umechongwa kwenye kipaji kile kile cha yule mwanadamu.

 Muhuri wa Jina la Baba ulioko kwenye kipaji cha uso inamaanisha kutembea katika ile hali ya kiungu, ambayo ni njia inayokubalika mbele zake Mungu; ; kwa jina hili pekee ndilo mwanadamu anaweza kwalo kujitwalia yaliyo yake Baba.Yeyote anayetafuta kuingia kwenye yale malango ya Ufalme wa Baba kwa jina lolote linguine atasimamishwa pale malangoni kwa usemi, “Sikujui, wewe mtenda maovu”. Kwa jinsi hii Roho asema, “je kuna mbwa”, na, “hakuna kitiacho najisi ama kisemacho uongo chaweza ingia uzimani”.

Ujue ya kwamba ramani halali na ya ukweli ni kwamba mwanadamu ni umbo na mfano wake Mungu; “na huu ndio mwanzo wa maumbile a Mungu”. Inamaanisha kuwa wanadamu wote kwa ukweli wana hali ya Baba imechongwa ndani ya uutu wao. Hii yaweaonekana nguvu kutafakari na hisia za kiwanadamu kwa sababu ya uchafu uliommeza mwanadamu, lakini yafungue macho yako na utaona hiyo hazina iliofichika ndani chombo hiki kinyonge na hafifu cha udongo.

Kiroho, unawezaifananisha kipaji cha uso na nia ya ndani ya mwanadamu; Roho anasema iweke kando nia ya kimwili na ukkaweze kubadilika na kufanana haswa na ile nia ya Kristo, ambayo ndio ya Mungu. Ukitaka kuuona uzima, kila mwanadamu lazima aweke nia ya kiwanadamu ambayo, kama lile joka la dunia ni chukizo dhidi ya Mungu, haliwezi kujua mambo ya ukweli wa umilele wa Mungu. Kuwa na nia ya kiwanadamu inaashiria kifo kwa sababu inamkinga mwanadamu kutokana na uhakika wa Ufalme wa Kiroho wa Mungu, usioonekana, kumfanya yeye kugaagaa kwenye giza, kunako wingi kilio na kusga meno. Upande wa pili, kipaji cha uso kilichochongwa Jina la Baba ni nia ya kiroho ya Kristo, ambayo, bila, hakuna mwanadamu ataona ukweli wa uzima wa milele na amani. Kwa Jina hili tu, mwanadamu anawezakuvumbua tena njia nyembamba na nyoofu iingiayo Shambani Edeni.

Warumi 8

6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitiisheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote aspokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 

 Sasa twawezaona kwa uhakika kuwa mwanadamu katika uasi wake anajiambatanisha nay a kidunia na huishia katika mtego wa hali ipitayo ya muda nay a wakati. Katika ile hali a uasi, mwanadamu hufanyika mfungwa wa uharibifu, anapouondokea ule uzima wake na hali yake ya kibingu, katika mfano wake Mungu aliye Muumbaji, na kuambatana na hali ya kilichoumbwa. Lakini neema imetujilia leo, kwamba kila mwanadamu anawezatizama mifano inayoonekana kupitia Yesu msalabani na ajue ya kwamba ni hali yake ya uanadamu, iliyodhoofika inayotiwa kifo msalabani, ili utukufu wa Mungu aishiye ikadhihirike. Kwa imani, wacha kila mwanadamu aisikiaye sauti ya Baba akainuke na kurejelea lile Jina Moja la Baba, kwa kuwa mtiifu kwa mwito wa kufa kwa mtu wa kale.


 

KUTEMBEA KATIKA JINA LA BABA

Nguvu ya kuweka hai na kupa uhai iko ndani ya Baba, na Baba amempa Mwana uwezo, kwa sababu Mwana hutembea katika Jina la Baba na hufanya lile tu alionalo Baba akifanya.

Yohana 5

20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu. 21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.

Yohana 5

25 Amin, amin, nawaambia, Saa inkuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.  26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafisini mwake.  27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwna wa Adamu.

Wanaoenenda katika jina la Baba ni wale waliomjua Mungu wa ukweli na aisjie, na kuishi kwa ajili Yake kuwapa Mkate na radhi waliopotea katika ulimwengu huu. (1 Yohana 2:13-14). Wao hufanyika wanaopeana uzima; wakiwa wameondolewa na kuangamizwa hali yao ya kijoka, inayotafuta maovu na mauti, ka hivyo kudhihirisha hali ya Baba Yao ambaye ni upendo na Uzima wa milele. Hawa, kati ya mia na arobaini na nne elfu wanaenenda kama Baba, wakiwaita wana waliotapakaa duniani humu kama yatima, kwa sababu wao wanafanyika Baba kwa wasio baba na Mama kwa wasio na mama.

Kristo aliyefufuka hii hali ya Baba iliyokuwa ndani mwake, alipowaita wanafunzi kula naye.

Yohana 21

5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La….9 Basi waliposhuka pwani, wakona huko moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate…12 Yesu akawaambia, Njoni mfumgue kinywa. Wala hakuna mtu katika wale wanafunzi aliyedhubutu kumwuliza, U nani wewe? Wakijua ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akautwaa mkate, akawapa, na samaki vivyo hivyo.

Yesu hakwenda sokoni kuutwaa mkate, wala hakwenda kutega samaki. Samaki waliokuwa makaani na mkate walitwaaliwa kutoka zile hazina za kimbingu ilizo ndani ya Baba; na ni Neno la Uzima.Ni Baba anawapa Mkate wa Ufalme wamawe ambao walikuwa wametawanywa kaika ziwa la wanadamu. Siku Mpya inapokucha, Baba anatokea na kuleta joto, kufariji na kutosheka katika mioyo ya wanadamu waliokata tama usiku kucha ndani ya shimo lililojaa mchafuko (ambalo ni ulimwengu huu ulio.)

Wanaohitimu mahali pale katika mlima ule mtakatifu, wanasimama kama Baba ulimwenguni, kama vile Yesu alivyosimama kama Baba wakati wa huduma yake. Basi mtu awezauliza, na si Yesu alisema usimwite yeyote baba ulimwenguni? (Mathayo 23:9). Ukweli ni kwamba, hawa walioko Mlimani Sayuni hawako duniani tena, mbali wako mawinguni na huishi kule; na sio wanadamu hafifu tena, kwa sababu walipotwaaliwa kutoka ulimwenguni (duniani), walifanyika viumbe vipya, vilivyofanyika kulingana na umbo la kimbingu ambalo ni Mungu Baba.

Kudhihirisha Baba ni huduma iliyokabidhiwa watakatifu naye Yesu, aliposema, Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. (Yohana 14:12).

Hapo mbeleni, Tomaso alikuwa amemwuuliza Yesu amdhihirishe Baba kwa wafuasi, na Yesu akawaambia peupe kwamba ni Baba waliyekuwa wakimwona; ilikuwa Mungu Baba alikuwa akijidhihirisha kupitia Mwana. Haya yote yanaenda kuonyeshakwama Yesu alitembea katika Jina la Baba, sio jina la mwanadamu hafifu. Hii ndiyo ile hali ya ukweli ya kila mwanadamu ambaye anahuishwa kuingia kweli, kwa sababu katika uhuisho huu, mwanadamu kwa hakika tena hufanyika dhihirisho la Mungu asiyeonekana hapa duniani.  "Alieniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?” (Yohana 14:9).

Hii haimanishi nikaenende jiani na mtaani na kupaza sauti, “Mimi ni Baba”, na pia haimaanishi nijitaalie neno Baba mbele ya jina langu. Huu nu ukweli tunaojihifadhia ndani mwetu na kumwacha Roho kuufunua huu ukweli kwa wanaotutazama. Wengine wetu wanawezashuhudia kuwa tumeingia mahali na makusanyiko ambapo hatukujulikana, lakini tupafichuliwa na watu waliotabiri, wakisema: “Baba wa mayatima”. Hii ni ishara ya mwito wa juu sana na umewekwa huru na bure kwa kila mwanadamu aliyetawanyika ulimwenguni huu.                


 

MABIKIRA NA MATOASHI ROHONI

Katika maono, waliotwaaliwa kutoka ulimwenguni wanaonekana Mlimani Sayuni kama bikira.Mafunzo na dini Fulani hufananisha hawa na watu Fulani spesheli ambao haajawahi fahamiana kingono na mwingine; dini zingine hutumia haya maandiko kuunda mafunzo yawakatazao watu – waume kwa wake kutooa. Twamshukuru Mungu kwa nuru ya ukweli wake ambayo hutokana na Roho wake katika siku hii. Kama umekumbana na hizi roho zinazopinda maandiko ili kutengeneza mafunzo yao potovu, wewe oma kile anasema kuhusu hawa bikira. 

Cha kwanza kutizama ni hiki, hawa walikuwa ni waume, ambao hawakujipaka najisi na wake, kwa hivyo ni bikira. Katika hali ya ukawaida, huwa ni tofauti, sivyo?  Kumaanisha, ni wake ambao hujulikana kama mabikira kwa kutojinajisi na wanaume. Inamaanisha kuwa hawa walikuwa wanaume ambao walifanyika matoasi kwa ajili ya Ufalme. (Kina dada wasomao hili, hawapaswi kuona kana kwamba nazungumzia wanaume kama vile wanavyojulikana ulimwenguni, kwa sababu hakuna kike wala kiume katika Kristo. Hicho kikundi cha mia na arobaini na nne elfu kina wana, kike na kiume ulimwenguni huu tulio).

Yesu alinena kwa ufupi kuhusu hawa wanaofanyika matoashi kwa ajili ya Ufalme: 

Mathayo 19

11 Lakini yeye akawaambia, “Si wote wawezao kulipokea neon hili, ila wale waliojaliwa. 12 Maana wako matoashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matoashi waliofanywa na watu kuwa matoashi; tena wako matosahi waliofanya kuwa matoashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neon hili, na alipokee."

 

Yesu kwa uhakika asema kwamba sio wote wanawezakubali haya isipokuwa waliojaliwa na kuchaguliwa. Yesu asema hivi kwa sababu alinena kwa lugha ya kiroho ambayo waliokombolewa wangeielewa.

Kunena kiroho, mabikira na matoashi (wanaume tasa) ni wale walioamua kujiweka kiroho na kutotiwa nira na mipango na mapambo ya kilimwengu wakati huu tulio. Hawa wamejiandaa kuolewa na Bwana na ufalme wake uliositirika pekee.  Nasema uliositirika, kwa sababu hali ya nia ya kimwili haiwezi kuuona huu ufalme wala kuuelewa. Mungu ni Roho na ufalme wake sio ule unaokuja kwa kutizama na hali za kimwili – ni kamili ufalme wa kiroho. Wanaousaka huu ufalme, lazima watembee kikamilifu wakiuzingatia ufalme wenyewe. Waliogizani hutembea kulingana na ulimwengu huu tulio, wa kijinsia na kimwili na wao husaka utukufu wa wanadamu na na ulimwengu huu ulio chini, lakini wale walio na na ufunuo hakika wa ufalme waMungu hutembea wakiwa na uhusiano na Baba ambay uwepo wake uko sirini,  ukiwa umefichika kutokana na watu wa enzi hii tunayoishi.

Huku ndiko kupanda katika roho ambako tumekusikia miaka hii yote, Mungu ni Roho; kutembea katika Mungu ni kupanda katika Roho. Hii ndio maan waona katika mistari fulani katika Ufunuo wa Yohana, sura ya kumi na nne, ikisema kuwa wao wanamfuata Mwana Kondoo popote aendapo.Macho saba ya huyu Mwana Kondoo humwona Baba pekee na ufalme wake na sio kingine chochote. Hawa mabikira wa kiroho wameunganika kwa Bwana kikamilifu na kwa hivyo hawana kauli yao wenyewe wala nia yao wenyewe, isipokuwa kufanya mapenzi ya aliye kichwa chao (Kristo), ambayo ni kumpendeza Mungu na kumpa utukufu yeye amabye kutoka kwake kila mema hutiririka.

Nabii Isaya pia akatabiri kuwahusu hawa mabikira wa kiroho (matoashi) wanaotafuta utukufu wa Mungu:

Isaya 56

1 Bwana asema hivi, “Shikeni hukumu, mkatende haki, kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa. 2 Heri afanyaye haya, namwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote." 3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, “Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake”; Wala toashi aseme; "Mimi ni mti mkavu." 4 Kwa maana Bwana awaambia hivi maoashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuna na wana na mabinti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.  6  Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafirahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote."

Unabii na kutabiri kwake Isaya ni neno la majira tulio sasa kwa wale mioyo yao inatia jitihada kuusaka ukombozi na wokovu wake Mungu; inaashiria watu wanaosaka kuwa kati ya wale 144000 walio Mlimani Sayuni. Hawa ndio watu, wanaouacha ulimwengu kuusaka utukufu wa Mungu; wanajiunganisha na Mungu kwa imani na wanatembea katikauhusiano kamilifu kwa Mungu wakitafuta kufanya kimpendezacho.  Isaya 58 yaendelea kueleza Sabato ni nini: inanena kuhusu kuunyima mwili anasa zake na kutenda kimpendezacho Mungu. Tunatimiza Sabato kwa kutembea hakika kwa Roho wa Kristo. Bila Roho wa Kristo kutuvuvia ndani mwetu, hatuwezihitimisha Sabato kamilifu ya Mungu; ni siku kuu ya Bwana, sio ya mwanadamu.

Siku zilizopita, watumishi walioaminika na waaminifu, ambao walikuwa na uwezo wa kuingia vyumba vya ndani vya wafalme na watu wakuu walikuwa matoashi. Kuwa toashi ilikuwa ni dhihirisho kwa mtumishi kuwa amejitolea kikamilifu kutumika na kumheshimu bwana wake kwa uaminifu. Haw matoashi walijikana vya kuwapa raha ili wampendeze mfalme pekee, na kwa sababu ya kauli hii ya kujitolea, walikuwa kwa kawaida wamekwezwa na kupewa kibali cha hata kuupenya uwepo wake mfalme, na hata kula kutoka chakula chenyewe cha mfalme.

Kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni, kwa ajili ya Yerusalemu, kwa ajili ya Sayuni, tumefanyika matoashi. Kama matoashi na mabikira, tumeziua hisia zetu za kimwili, nia zetu, vitupendezavyo, kusaka tu kimleteacho Bwana wetu (ambaye ni Roho) raha, kumpa heshima pekee; na tunapofanya hivi, Bwana aahidi kutuleta kwa Mlima wake Mtakatifu ambapo anatuahidi raha hata milele yote. Atuahidi sisi jina la umilele na kilele cha furaha Mlimani wake Mtakatifu Sayuni. Hilo jina ni jina jipya – Jina la Baba.

Siku huja ambapo mwanadamu huanza kwa uhakika kupendezwa na mambo yanayoambatana naye Bwana, asilegezwe tena na raha za mambo ya kimwili. Wale wanajitalaki kutokana na raha za kimwili na kugundika na kushikamana na maisha ya Roho, watasafirishwa mpaka sehemu ya furaha isiyoisha kwenye vilele vya Sayuni. 


 

WAMFUATA MWANA KONDOO KOKOTE AENDAKO

Kama kondoo waufuatavyo unjia aupitao mchungaji, hawa walio Mlimani Sayuni humfuata Mwana Kondoo kokote aendako, kumaanisha kuwa wanaongozwa na Roho wa Mungu. Mtu awezajiuliza, "huyu Mwana Kondoo awaongoza awaelekeza wapi?” Mwana Kondoo awaelekeza kurudi katika uwepo mtukufu wa Baba mahali ambapo wanaweza tena ishi uzima wa kweli ulioko ndani yake Baba. Wakati Yesu mara kwa mara alipokiri, “Naenda kwa Baba”, ulikuwa ni upako ulioko ndani mwake – uitwao Kristo, ulikuwa ukieleza makusudi Yake. Sauti iliyokuwa ikisema, “Nifuateni Mimi”,  ilikuwa ni sauti ya upako ulioko ndani uliokuwa ukimwita mwanadamu muasi kuurejelea Utukufu wa Baba.

“Nilipo, watumishi wangu wawepo”, kama mchungji, Mwanakondoo aziongoz nafsi za wanadamu kwenye chemichemi za mji ya uzima mahali ambapo hawaoni kiu tena wala kukosa lolote. Katika hali y kawaida ulimwenguni tulioko, wanadamu katika umbo la wachungaji wa kondoo huwaongoza wanakondoo kuelekea  kwa majani mabichi, lakini katika maono ya huyu mtume, twayaona haya ni kama yamepinda. Twaona Mwnakondoo akiwangoza wanadamu kuelekea kwa Uwepo wa Mungu. Hili ni dhibitisho vile hekima ya Mungu huwa ni kama upuuzi tu kwa wanadamu wa majira tunayoishi wanaoyaona mambo kwa roho tu ya kiasili. 

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni. (1 Wakorintho 2:14)

Kwake Mwanakondoo wa Mungu (Roho wa Kristo aliye ndani) ni hekima yote ya kiroho na maarifa yake Mungu. Yohana alipomwona (Mwanakondoo) mbele ya Kiti cha Enzi chake Mungu, alikuwa nayo macho saba yakiashiria Roho Saba zake Mungu zilizotumwa ulimwenguni.

Ufunuo wa Yohana 5:6. Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wane, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

Hizi Roho saba za Mungu zaashiria hekima iliyotwaaliwa kutoka vilindi vyake Mungu, na kutumwa duniani kote kuwanusuru na kukomboa wanadamu kutoka ulimwenguni. Dunia yenyewe ni kiashiria cha kiroho kuonyesha ulingo wa mavumbi mahali ambapo kifo na kuzimu hutamalaki. Hizi Roho saba huwanusuru hawa kwa kuwachapa muhuri vipaji vya nyuso (nia) za wanadamu na kuwatia nuru kuwaingiza katika nia ya juu zaidi ya Aliye Kweli ambayo hujaa kila kitu Naye Yeye Mwenyewe.

Hizi Roho saba zawakilisha fani nyingi za hekima yake Mungu zilizotolewa kilindini chake Mungu, na kutumwa duniani ili kuwanusuru wanadamu kutoka ulimwenguni. Dunia yenyewe kwa hakika ni ishara ya kiroho ya hali ya uvumbi ambapo gehena au jehanum na kifo hutamalaki. Hivi vitu na hali hufanya hivi kwa kuchapa muhuri kipaji (nia) ya wanadamu na kuwaangazia kuingia katika dhamiri ya juu zaidi ya Yule aliye Kweli, Asiyeonekana, na ajaaye vitu vyote kwa vyote.

Mwana Kondoo, anayewakilishwa na Kristo Aliye ndani, huishi ndani ya kila mwanadamu ambaye tu atakkubaliana na ukweli wa hali hii, na Yeye Ndiye yale Mafuta na Sauti iongozayo, inayoelekeza wana wa Ufalme kurejea katika hali ya kukubali kuwa wanashiriki katika Utukufu wake Mungu. Inamfunza mwanadamu kweli zote na hubaki ikiwa karama iliyo kuu zaidi yake Mungu kwao wanadamu, kwa sababu bila Roho, hakuna mwanadamu anawezatambua hali yake ya kweli katika Utukufu wake Mungu. Kila mmoja wa hawa asimamaye Mlimani Mtakatifu wa Mungu, Sayuni, hufunzwa naye Mungu kupitia Yale Mafuta yaliyoko ndani mwao.

1 Johana 2

27  Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.

 

Isaya 54

 

13  Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

 Wanaosaka na kutafuta mahali hapa pa uzima inawalazimu kuyatoa macho yao ya ufahamu na kuyatia yale Yake Roho. Lazima waukate uguu wao uwaongozao kusiko na waweze kutembea kwa mwongozo Wake Roho.

 

Mathayo 18

8 Basi mkono wako au mguu wakoikikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.

9 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.

Yale macho sba ya Mwna Kondoo hufanyika macho yao ya ufahamu yawaongozayo mahali ambapo hakuna mwanadamu wa kiasili apaelewa wala kuwezeshwa kupaelewa. Hawa wabarikiwa huoneka na huhukumiwa na wana wa kizazi hiiki kuwa wajinga, lkini wao kwa hakika ni wenye hekima kwa sababu wanasimama katika mahali palipoinuka, kuutazama utukufu uliokamilika wake Mungu.

 

Isaya 35

8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.

9 Hapo hapatakuwa na samba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.

10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitkimbia.

 

Njia ya utakatifu katika hali hii ni njia tofauti, mpya nay a uima ya kuishi ambayo Baba ameiwakifisha wanadamu wote wakaipitie. Katika njia hii ya utakatifu, Aliyeko pale ni Bwana na Bwana Pekee. Wanaotembelea njia hii waishi pekee kwa Roho. Hli nyingine yoyote hufanyika najisi, kikwazo, na idanganyayo; kilicho najisi na kichafu, kifanananishwacho na samba araruwaye na kula. Hawa wanyama wote ni viashirio vya hali isiyotakasika ya mwanadamu wa aili anayeishi kulingana na au kuambatana na hali ya Adamu, ya damu na nyama. Hakuna njia yeyote ambayo damu na nyama huweza kuona wala kutambua ufalme uliobarikiwa, uliositirika wa Mungu, kuna ulazima wake yeye kuzaliwa kiroho kupitia kufanyika upya nia yake. Ndio aweze kuishi, inambidi mwanadamu kuingoa hali hii yake ya kuishi ya kinyama na kujitwalia Roho wa Mungu; inambidi aone pekee kwa macho ya Mwana Kondoo aliye ndani yake ambaye humwona tu Baba.

 

Mwanadamu amfuatapo Mwana Kondoo, hii humpeleka katika hatua ya kuzaliwa upya ama kufanyika upya (katika nia) ndio ile mbegu takatifu isiyo mawaa iliyo katika mfano wa Bwana wake itokee. Hapa ndipo mahali pa waliokombolewa; wao huja mahali ambapo kila hali ndani mwao hujipanga na kujisawazisha kikamilifu sambamba na Roho wa Mungu. Kwa Roho, ile hali najisi ya kinyama iliyokuwemo ndani ya uzao huu spesheli, pamoja na uchungu na hofu ya matukio ya kiwanadamu hutokomea mbali, ni kana kama huyu mwanadamu amegutuliwa kutoka kwa ndoto chafu na ishtuayo; wanaupokea uridhi wa milele, furaha iishio ya Mungu wao.

 

 

 


 

HAWAGAIRI, KUSEMA UONGO NA HUSIMAMA BILA HUKUMU MBELE YA KITI CHA ENZI

Kabla tuanze kutambua maana ya Uongo, wacha tukaweze kuelewa watu wawili wanaoonekana kuanzia siku za Adamu na Yule aliyetoka mbinguni ayulikanaye kama Adamu wa pili - Kristo. Wacha tutambue ukweli kuwa mwanadamu pale mwanzo aliumbika kwa Mfano wake Mungu; huu mfano ni wa kiroho na usiounganika kimwili. Kuungamanika kwa mwanadamu kiushirika na yule nyoka ndicho chanzo cha mwanadamu wa kimwilitunayemuona siku hii tulio duniani. Nyoka mwenyewe ni mfano wa fikra na nia za kimwili ambazo kila wakati zimeshikamana na kugundika na ulimwengu; ni fikra ambazo haziambatani na mambo ya kiroho ya Mungu. Huo umbo asili katika mfano wa Mungu walinganika na “Chanzo cha maumbile ya Mungu”, ama kwa maneno mengine, “Ukweli”. Uongo huja kupinga na kushusha kweli iliyoko, na tunawezasema kuupinda ukweli. Wakati mwanadamu anapopotea kutoka kwenye ramani ya kiungu na kuegemea kilicho cha jinsia na cha kidunia, uongo hujitokeza, na pamoja na ule uongo huja shida na dhiki zinazotokana na uhai uliotengeka na Yule ambaye ni Mungu wa kweli.

Kristo ndiye Mfano wa Mungu aishie, Yeye aliye kutoka Mwanzo; na hili ni dhihirisho la Uzima na Uhai ulio wa kweli na hali ya kila mwanadamu hata ingawa kwa muda mwanadamu yule anawezakuwa amepungukiwa na ile kweli kuu. Huu ukweli umefichika ndani ya kila mwanadamu katika hali ya uhai wake. Paulo analenga hili na anaiita hazina isiyohesabika, ya dhamana, iliyofichika katika vyombo vya udongo. Ufunuo huu wa nuru unang'aa leo kupitia Roho kuufunua huu ukweli ili mwanadamu anaweza tena kurejeshwa katika ule ushirika usiotengeka na Baba. Lango kuu la kurejelea katika kuungamanika huku na Mungu ni mwanadamu kuamka kutoka usingizi wake na kuutambua ukweli kuwa Kristo yu ndani mwake. Na ndio maana Shahidi aliye ndani asema,  “Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi”. Roho amwelimisha mwanadamu kuhusu chanzo chake katika Mwili wake Kristo na sehemu yake yule mwanadamu katika Ule Mwili; na huu ndio Uzima wa Milele.

1 Yohana 5

20  Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.

Uhai unaofuata mwili ndio uongo na ndicho chanzo cha uovu na upotovu wote ulioko leo, na ndio maana Yesu asema, “Usiusumbukie uhai wako kwa sababu wote ni bure”. Hakuna njia yoyote mwanadamu aishie kulingana na  mwili na damu awezasimama bila chachu wala mawaa katika uwepo na utukufu wa Mungu, kwa sababu, katika hali yake, yeye ni muasi na ni kiwiliwili tu cha umbo wa fikra zake. Mwanadamu yeyote atembeaye kulingana na mwili na anaungama maisha yaambatanayo na mwili ni muongo; yeye anaishi katika udanganyifu. Kwa jinsi hii, nikinena kiroho, wanadamu wote huwa na hufanyika waongo.

Zaburi 116

11 Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo.

Kama, kwa upande wa pili, mwanadamu anawezasikia manukato ya kuongea kwake Roho na kuambatana na yale yasemwayo, kumfuata Mwana Kondoo popote aendako, yeye ataujua ukweli na huu ukweli humfungua na kumuweka huru kutokana na nira na pingu za kifo. Kweli ni kwamba, utambilisho wa mwanadamu halisi ambao ni Kristo, bila chachu, utambulisho uliofichika ndani ya Mungu; utambulisho mwanadamu aliupoteza na kupokea gharika ya uongo na giza ya ulimwengu tuliomo.

Wasimamao wakiwa wamekombolewa Mlimani Sayuni hawana uongo mdomoni mwao kwa sababu wao huungama na kunena kweli tu kutokana na Nia Yake Roho, sio kulingana na nia ya mwili.

Ufunguo wa kweli unaowaondolea wanadamu lawama mbele ya Kiti cha Enzi ni imani ndani ya damu ya Mwana Kondoo na kutambua mbegu halisi na ya kweli na ile hali ya kweli ndani mwake. Wakati umekuja na umewadia wa kutambua mbegu hii takatifu ndani ya kila mwanadamu na kuacha kutambua wanadamu kulingana na mwili na damu, kwa sababu, tuendeleapo kutambuana kulingana na mwili na damu, wanadamu hupoteza kuona kwake kwa ule ukweli na kutumbukia kwenye mtego wa kifo. Ndio maana Mtume asema:

2 Wakorintho 5

16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sis tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.

Ufunguo wa kuzitwaa nguvu, mamlaka na imani mbele zake Mungu ni nguvu za dhamiri isiyonajisika na kuondolewa lawama kabisa mbele zake Baba. Hili huja kwanza kupitia mwanadamu kupambanua kweli, na uwezo wake kuzipungia kwaheri sauti zote zipingazo kweli na imani na kutembea katika kweli. kwa kujua kweli kumhusu yeye, kama Kristo, atakiri, “Mimi na Baba ni Mmoja, na ni Kiungu kisichotengana”. 

Kinachodanganya dhidi ya kweli hubaki nje ya lile Jiji la Dhahabu mahali ambapo wasiomjua Mungu huangamia kwa sababu ya upumbavu ulio ndani ya mioyo yao unaowatenganisha na Uhai na Uzima ulioko ndani ya Mungu. Wakati umewadia na ndio huu tulio, ambapo mwanadamu akaujue ukweli na kuukariri ndani mwake na kwa kila mwanadamu mwingine; kwa sababu hili hufungua Malango ya Milele kuingia kwao Ufalme wake Mungu.

Waefeso 4

25  Basi uvueni uongo, mkasemekweli kila mtu kwa jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.


 

WIMBO MPYA MBELE YA KITI CHA ENZI

Hebu keti na kutafakari kwaya ya kimbingu na nzumari na zeze na sanaa za nyuzi, wakiimba nyimbo zilizo na ukuu na uzuri wa kimbingu, ambazo hazijawahisikika ulimwengu tuliomo. Hiki kikundi cha waliokombolewa wanaimba wimbo mpya amabo hakuna mwanadamu angewezafunzwa, isipokuwa wale waliokombolewa kutoka ulimwenguni. Najua kwamba kila mwanadamu atafuta kuwa katika ile hisabu ya waliokombolewa. Ukweli ni kuwa, mtu yeyote awezasimama katika ile hesabu, muda tu anapochukua ujumbe huu wa Neema na kukimbia nao katika uwepo wake Mungu.

Huu ni wimbo wa ushindikuwa wale kwenye hii hali ya Utukufu wawezauimba; hawa ndio ndio wanaowezaimba,  “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”, "Bwana ni mchungaji wangu, sitapungukiwa kitu", “Bwana ameikomboa nafsi yangu kutoka shimoni na nitaona Nuru Yake”, “Amenifanya kuwa na furaha kuu”.

Wasimamao Mlimani Sayuni, Eneo la kiroho lake Mungu lililoinuka, wana macho yao yamefunguliwa kuuona utukufu na urembo wa Yeye Aliye Wa Kweli na wanapata kujua na kushiriki vilindi vya upendo wa Mungu. Sawia na pamoja, vinubi, zeze na nzumari ndani mwao zafunuliwa pamoja na maumbile mengine yote kutangaza rehema zake Mungu zisizotajika toka kizazi hadi kizazi.

Mtu awezatamani kuuliza, “Kama wimbo ulio kwenye vinywa vya waliokombolewa ni wimbo mpya, wimbo uliokuweko, ule mzee, ni upi”? Wimbo mzee unazungumzia kuomboleza na kilio, kusaga meno na dhiki kuu katika ulimwengu wa wafu ambapo mwanadamu aliuweka utanda wake na kulala pale, kwa kutofahamu. Haya yote yanawezafupishwa na kuwa mstari mmoja, na ndio huu, “kutengwa na ule Uhai na Uzima ambao Ndio, na uliohifadhika ndani yake Baba Mungu”.

Msomaji wangu, inuka na udhihirishe ile nuru ambayo wewe ndiye, leo ndio siku yako ya ukombozi na kufufuka katika na kuingia utukufu wako. Sikiza, sikiza, elewa na uchanganye maneno haya yaliyotakasika na imani na utatambua tena mtu wa Mungu ambaye uliye. Unapojitembua tena vileleni vya Sayuni, utapepea juu ya vyote na kutawala vyote. Zeze iliyoko ndani mwako ambayo iliwekwa chini kingoni mwa mito ya Babeli ikawezeinuka tena katika mfano wake Mungu, ikatamalaki katika ukamilifu, Utakatifu, na bila lawama, kwa sifa za Utukufu Wake.

Zaburi 137

1 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.

2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.

3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

Kusifu kwa kweli hakupatikani kati ya wanadamu wa ulimwengu huu, hata kuwe na kusifiwa na hisia gani, ni bure, na ni maigizo tu ya kidini ya wanadamu watembeao katika vivuli vya giza. Ndio, kuna uwezekano kuwa wewe wawezainuliwa na zile hali, lakini kila mwanadamu na afahamu kwamba hii sio hatimisho ya kile ambacho Mungu ameweka ndani ya mwanadamu. Sis sio wasimamao na kuwakashifu wanadamu, ila sisi huwasihi watu wote kupaa na kukwea na Bwana katika kufufuliwa kwao, kuhisi kuabudu kwa kweli kwa kimbingu. Ni kwa kweli, kwa kusisimua na kusikoelezeka kwa usemi wa mwanadamu. NI KWA AJABU!!! Sababu yake ni kuwa kila chembe ya uhai ndani ya mwili wa mwanadamu inaambatanika na maumbile mengine ulimwenguni huu kumtukuza Yeye Aliye Juu ya vyote.

Sifa yapatikana katika Jiji Takatifu Lake Mungu, ambalo ni Yerusalemu ya Kimbingu, Jiji lililowekwa kwenye vilele vya Sayuni. Hatusemi kuhusu zana za nyuzi za kijinsia bali zana za nyimbo za kiroho zilizoko ndani ya mwanadamu. Wasimamao kati ya wale 144000 wanamwimbia Bwana kwa hali ambayo wale tu walioko kwenye nuru wanaweza elewa pekee. Kwa hakika, ni kama nuru na rangi zake saba, wimbo katika hali ya kawaida una sauti saba; na hizi ni ishara na mifano iashiriayo nuru na kuelewa kunakotokana na Roho Saba zake Mungu. Hawa ndio wanaowezauimba ule wimbo, ambao wamefufuka kwa na kuishi kwa Roho wa Kristo ndani yao na ndimi zao zimefunguka kupitia Roho kuona na kukiri maono ya kimbingu.

Zaburi 57

8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.

Rafiki zangu, upendo gani na heshima gani inayoweza kuwepo kuliko ukuu huu wa wokovu wa Mungu unaoletwa kwetu kwa sahani ya dhahabu – kwa heshima kuu vile. Wokovu ambao humrusha mwanadamu hadi kilele cha maumbile na kumfanya yeye kutembea kama Mungu machoni pa Ulimwengu!

 

Bwana na akulinde.

Trevor Eghagha